Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho, aeleza sababu ya kuachana na mume wake
Baada ya tetesi za muda mrefu, inasemekana kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania, ameachana na mume wake Pastor John Shusho.
Tetesi hizo zilianza kuibuka pale ambapo mwimbaji huyo maarufu alipoacha kuhudhuria kanisa la mume wake na kuanzisha la kwake ambalo amelipatia jina la "Dream Center" ambalo bado lipo likiendelea na ujenzi.
Mama huyo pia amekuwa akionekana bila pete yake ya ndoa, jambo ambalo limeendelea kuibua maswali mengi kwa watu. Akiwa anaongelea jambo hilo kwa mara ya kwanza, mwimbaji huyo alisema kuwa
"Ukweli ni kwamba ni assignment tu there is nothing more than that. Ni assignment tu ambayo nimekuta Mungu amenipa kipindi hiki. Kwa hiyo lazima nitoke niende ku fulfill assignment,” Shusho alisema.
Pia aliongeza kuwa kabla ya yeye kuchukua uamuzi wa kuanzisha kanisa hilo, walijadiliana jambo hilo na mume wake na yeye ndiye aliyemruhusu kuendelea nalo.
Alipoulizwa ni kwanini ameacha kupost picha za mumewe kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na Facebook, alisema kuwa jambo hilo halimuingizii pesa yoyote ndio maana haendelei kupost.
"Siposti picha ya familia yangu sababu haileti pesa. If it doesn’t bring anything why post?”
No comments