Japan washibana nguvu na Senegal
Katika mzunguko wa pili wa kundi H, Japan waliweza kushibana nguvu na Senegal katika mechi ya kukata na shoka ambapo mchezo huo uliweza kuisha kwa mabao 2-2. Bao la kwanza liliweza kufungwa na Sadio Mane mnamo dk ya 11' ya mchezo na Takashi Inui aliweza kusawazisha bao hilo mnamo dk ya 34' ya mchezo.
Katika kipindi cha pili, Senegal bado walionekana na nia ya kutaka kuipeperusha bendera ya Afrika na kuongeza matumaini kwa bara hilo walipopata bao kutoka kwa Moussa Wague dk ya 71' lakini haikuwa muda mrefu na bao hilo lilirudishwa na Keisuke Honda dk ya 78' ya mchezo akiwa ametokea benchi.
Sasa Japan na Senegal wote watakuwa na point 4 baada ya timu zote hizo mbili kushinda katika michezo yao ya kwanza, na kutoa sare katika mechi yao ya pili.
No comments