Polisi wamsaka mshukiwa wa shambulio la Ugaidi, Ufaransa
Watu wawili wamekufa na wengine 12 kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kwa risasi eneo lililokaribu na soko la Krismass mashariki mwa mji wa Strasbourg, Ufaransa.
Mshambuliaji huyo ambaye anajulikana na vyombo vya ulinzi, anasakwa na polisi baada ya kukimbia akiwa amejeruhiwa wakati akipambana na polisi kwenye tukio hilo. Shambulio hilo limetokea karibu kabisa na soko la Krismass lenye shughuli nyingi, ambalo limekuwa kivutio cha maelfu ya watalii, katika msimu huu wa sikukuu.
![]() |
| picha yaonesha eneo la tukio |
Mwendesha mashtaka wa kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Ufaransa ameanzisha uchunguzi wa tukio hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Christophe Castaner ambaye amethibitisha vifo hivyo, amelielezea tukio hilo kama hatari kiusalama.
Watu sita kati ya waliojeruhiwa wameelezwa kuwa katika hali mbaya. Polisi wanasema mshukiwa wa tukio hilo mwenye ujmri wa miaka 29, tayari anajulikana na vyombo vya ulinzi na kuna uwezekano wa kuwa ni tukio la kigaidi.
Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, mtuhumiwa huyo ambaye amekimbia nyumbani kwake amekuwa akitafutwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.


No comments