CAF yatarajia kuahirisha mashindano ya AFCON hadi kufikia 2021
Shirikisho la soka barani Africa (CAF) limesema kuwa linatarajia kusogeza mbele mashindano ya kombe la mataifa ya Africa mpaka itakapifika mwakani 2021 kutokana na sababu mbalimbali na changamoto, ikiwemo corona, wakati ambapo michuano hiyo ilibidi ianze mwezi Oktoba kwa mechi za kufuzu.
Mashindano hayo, ni moja kati ya mashindano makubwa barani Africa kwa mpira wa miguu na wanamichezo wote. Huwa yanashindanisha mataifa 24 kila baada ya miaka 2.
Mashindano yote ya mpira wa miguu barani Africa na duniani kote yalikuwa yamezuiliwa kwa muda wa miezi mitatu kutokana na janga la corona, jambo ambalo lilizuia ratiba ya mechi za kufuzu kwa kombe hilo ambazo ratiba yake huwa ni mwezi March na june.
No comments