Breaking News

Asilimia 85 ya bunduki bilioni moja duniani zinamilikiwa na raia

Ripoti inayotolewa kila mwaka na shirika angalizi kuhusu silaha ndogo imesema takriban asilimia 85 ya bunduki zaidi ya bilioni moja duniani zinamilikiwa na raia huku Marekani ikiwa na idadi kubwa ya raia wanaomiliki bunduki, ikikadiriwa kuwa kuna bunduki 120 kati ya kila raia 100 nchini humo. 

Raia hao wa Marekani wanamiliki zaidi ya asilimia 40 ya bunduki na bastola bilioni moja zilizoko duniani ikifuatiwa na Yemen ambako kati ya raia 100, kuna bunduki 53. Nchi nyingine zilizo katika orodha hiyo ni Montenegro, Indonesia, Japan na Malawi. Kulingana na ripoti hiyo ni asilimia 13 pekee ya bunduki na bastola zilizo mikononi mwa wanajeshi na maafisa wa usalama.

No comments