Trump aapa Marekani haitageuzwa kambi ya wakimbizi
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump unazidi kushutumiwa kuhusiana na sera yake kuhusu wahamiaji ambayo imepelekea maelfu ya wazazi kutenganishwa na watoto wao mipakani.
Trump ambaye amewashutumu Wademocrats kwa sera hiyo iliyowatenganisha watoto 2,000 na wazazi wao katika kipindi cha wiki sita zilizopita, ameonya kuwa wahamiaji wanaweza kuwa wauaji, wezi na wahalifu wengine na kusisitiza kuwa Marekani kamwe haiwezi kuwa kambi ya wahamiaji au kituo cha kuwashikilia wakimbizi, akitolea mfano wa Ulaya alikodai wahamiaji na wakimbizi wametatiza hali ya kawaida ya maisha.
Awali, alidai kuwa viwango vya uhalifu Ujerumani vimeongezeka kutokana na sera ya kuwaruhusu zaidi ya wahamiaji milioni moja kuingia nchini humo mwaka 2015.
No comments