Breaking News

Idadi ya waliojeruhiwa katika mripuko Addis Ababa ni 83

Watu 83 wamejeruhiwa katika mripuko wa guruneti kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara, wa waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwenye mji mkuu wa taifa hilo. 

Abiy alikuwa amehitisha hotuba yake katikati mwa Addis Ababa mbele ya maelfu ya wafuasi wake, wakati mripuko ulipotokea na kusababisha waziri mkuu huyo kuondolewa eneo hilo kwa haraka. 

Katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televisheni muda mchache baadaye, Abiy amesema shambulio hilo limetekelezwa na makundi yaliyotaka kuhujumu mkutano huo lakini hakuyataja. 

Awali, Abiy alisema watu kadhaa walikuwa wameuawa lakini baadaye mkuu wake wa utumishi aliandika kupitia ukurasa wa Titter akisema idadi ya waliojeruhiwa inafikia 83 na kifo cha mtu mmoja.

No comments