Breaking News

Marekani yamuwekea vikwazo Rais wa Syria Assad na mkewe

Marekani imewawekea vikwazo watu na makampuni 39 akiwemo Rais wa Syria, Bashar al-Assad na mkewe Asma vya kuzuia mapato ya serikali yake katika jitihada ya kuishinikiza Syria kurejea katika mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo amesema vikwazo vingine vingi zaidi vinapaswa kutarajiwa dhidi ya serikali ya Assad katika wiki na miezi ijayo.

Vikwazo hivyo vimewekwa chini ya Sheria ya Kaisari ya Kuwalinda Raia wa Syria iliyopitishwa na Bunge la Marekani Desemba mwaka jana na kuidhinishwa na Rais Trump.

Wakati vikwazo vya awali vya Marekani viliilenga zaidi serikali ya Syria, sheria hii mpya pia inawaadhibu watu, taasisi na makampuni ya Syria na ya kigeni yanayounga mkono shughuli za kijeshi nchini Syria zinazofaynwa na washirika wa al-Assad - ni Urusi, Iran na kundi la Hezbollah nchini Lebanon, ambao wamekuwa wakiisadia serikali hiyo kupigana na makundi ya upinzani.

No comments