Kombe la Dunia 2018: Neymar apata jeraha na kutoka katika mazoezi ya Brazil
Mshambuliaji wa Brazil Neymar alilazimika kutoka katika mazoezi ya kikosi cha Brazil siku tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Costa Rica siku ya Ijumaa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alirudi kutoka katika jeraha la mguu uliokuwa umvunjika alijiondoa katika mazoezi ili kupata matibabu ya kifundo chake cha mguu.
Msemaji wa Brazil alihusisha jeraha hilo na mechi ya Switzerland ambapo mchezaji huyo alichezewa visivyo. ''Mara tu alipohisi uchungu, alienda kwa daktari wa maungo'' , alisema Vinicius Rodrigues.
"Atasalia huko kwa leo na kesho alfajiri na atafanya mazoezi kama kawaida kesho.
Kiungo huyo wa Paris St-Germain alifanyiwa upasuaji katika mguu wake wa kulia mnamo mwezi februari na kumfanya kukosa msimu wote uliosalia .
Alirudi kuichezea Brazil katika mechi ya kirafiki dhidi ya Croatia mjini Liverpool tarehe 3 mwezi Juni na kufunga bao zuri.
Alifunga tena katika mechi ya kirafiki ya mwisho dhidi ya Austria ambapo Brazil ilipata ushindi wa 3-0 kabla ya kikosi hicho cha Tite kuelekea Urusi.
Neymar alicheza dakika 90 za Brazil katika kundi E dhidi ya Switzerland ,lakini hakuonekana katika mazoezi siku ya Jumatatu katika kambi yao iliopo Sochi.
Brazil inakutana na Costa Rica katika mji wa St Petersburg siku ya Ijumaa.
Mwaka 2014 kampeni ya kombe la dunia ya Neymar ilisitishwa na maumivu ya mgongo katika mechi ya ushindi ya robo fainali dhidi ya Colombia
No comments