Tetesi za soka barani Ulaya 20.06.2018
Ajenti wa Maurizio Sarri amewasili London na meneja huyo wa zamani wa Napoli mwenye miaka 59 ambaye anatarajiwa kuchukua mahala pake Antonio Conte kama meneja wa Chelsea. (Sky Sports)
Crystal Palace watampa ofa Wilfried Zaha ya puni milioni 120,000 kwa wiki kumzuia raia huyo wa Ivory Coast mweye miaka 25 ambaye ameivutia Tottenham. (Mirror)
Huddersfield wanatarajia kuwashinda Southampton na Lyon katika kumsaini mshambuliaji wa Ubelgiji kiungo wa kati Anthony Limbombe, 23, kutoka Brugge. (Sun)
West Brom wamekataa ofa ya kwanza ya Burley kwa mchezaji Jay Rodriguez, huku mshambuji huyo mwenye mika 28 akitarajiwa kurudi kwenye klabu yake ya zamani. (Mail)
West Ham na Burnley wanashindana kumsaini mchezaji wa thamani ya pauni milioni 8 msenegal Moussa Konate, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Ligue 1 Amiens. (Sun)
Southampton wanajiandaa kumwendea kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg ambaye ni raia wa Mali Amadou Haidara, 20. (Mirror)
Tottenham wanafuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Lyon mfaransa Tanguy Ndombele, lakini hawajazungumza na klabu hiyo ya Ligue 1. (Sky Sports)
Marseille wanamtaka mchezaji wa miaka 29 wa Everton raia wa Ufaransa Morgan Schneiderlin, ambaye ameambiwa kuwa anaweza kuondoka Goodison Park. (France Football, via Tribal Football)
Newcastle ni lazima washindane na Bayern Munich kumsaini kiungo wa kati wa Hoffenheim raia wa Croatia Andrej Kramaric, 27. (TZ, via Talksport)
Mazungumzo yameendelea na Roma na West Ham kuhusu kiungo wa kati wa Argentina Javier Pastore 28. (ESPN)
Wing'a wa Wolves mreno Ivan Cavaleiro, 24, hana nia ya kuondoka Molineux licha ya kuhusishwa na kuhamia huko Huddersfield. (Birmingham Mail)
No comments