Breaking News

Mashabiki wamjia juu Eminem


Rapper kutokea nchini Marekani Eminem, ameingia kwenye mgogoro na mashabiki wake kuhusiana na show aliyofanya Jumamosi katika uwanja wa Bonnaroo.

Mashabiki wengi walisikika wakipiga kelele katika show hiyo wakimshamgilia msanii huyo lakini ghafla ukasikika mlio mkubwa sana mfano wa bunduki ambao uliwashtua watu wengi na hata wengine wakaanza kutawanyika kwa kudhani kuwa yameanza mashambulio ya bunduki.

Mashabiki wengi walimlaumu sana mwanamuziki huyo kwani kufuatia matukio mengi sana yanayotokea nchini humo, yakiwemo kuuawa kwa watu weusi sababu ya ubaguzi wa rangi, hivyo tukio hilo la yeye kupiga mlio huo wa bunduki uliwakosesha amani watu wengi na kumtaka kutorudia tena.

No comments