Guadiola: Yaya Toure ni muongo, sijawahi kuwa na tatizo na wachezaji weusi
Kocha wa klabu ya Manchester City iliyoko jijini London, amekanusha kauli ya mchezaji wake wa zamani "Yaya Touré" ya kusema kuwa kocha huyo hapendi wachezaji weusi, na kusema kuwa jambo hilo ni la uongo.
Touré aliyasema hayo kwenye interview moja jijini London, baada ya kuwa amehusishwa kwenye kikosi hiko mara moja tu kwenye "First Eleven" ya timu hiyo kwa msimu mzima. Toure alisema kwamba kocha huyo huenda akawa na matatizo nae kwani si mara ya kwanza kwa yeye kumfanyia mambo kama hayo kwani tangu walipokuwa wote Barcelona bado alikuwa anafanya hivyo.
Guardiola alikanusha maneno hayo na kusema kuwa hajawahi kuwa na tatizo na wachezaji wenye asili ya kiafrika na kusema kwamba walikuwa wote kwa miaka miwili kwanini hakuwa kumwambia wakiwa ana kwa ana?
Yaya Toure mwenye umri wa miaka 35 ameshinda kombe la ligi kuu ya Uingereza mara tatu, kombe la FA na kombe la Capital One katika miaka yake nane aliyokaa Etihad na kusema kwanza yeye sio mtu wa kwanza kumuongelea kocha huyo kuhusu tabia yake hiyo.
Nawafahamu baadhi ya watu Barcelona hata hapa Etihad ambao wanafahamu jambo hilo, labda kwasababu sisi ni wachezaji weusi na tunafahamu kuwa sio kila mtu ataweza kutuhudumia vizuri kama watu wengine wote wanavyofanyiwa.


No comments