Breaking News

Rapper XXXTentacion afariki kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 20


Moja kati ya wasanii wa muziki wa HipHop wanaochipukia kwa sasa akiwa na umri wa miaka 20 ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 20. 


XXXTentacion aliuawa siku ya Jumatatu mchana katika mji wa Florida nchini Marekani. Kituo cha polisi cha Broward kiliweza kudhihirisha jambo hilo kupitia kwenye ukurasa wao wa Twitter baada ya kueleza kwamba, rapper huyo mwenye jina halisi (Jahseh Onfroy) aliweza kupatwa na mauti baada ya kufikishwa hospitali. 

Vyombo vya usalama viliongea na E News!! na kuelezea kwamba vita hiyo ya bunduki ilitokea katika beach ya Deerfield mnamo saa 9:57 mchana. Msanii huyo alikuwa akiondoka RIVA Motorsports wakati watu wapatao wawili wenye silaha walipofuata gari la msanii huyo na mmoja wao kupiga risasi kabla ya wawili hao kuondoka na gari nyeusi aina ya SUV na kuelekea mahala pasipojulikana. Mamlaka zinaendelea kufanya uchunguzi wa suala hilo. 


Video zinazosambaa mtandaoni hivi sasa, zinamuonyesha kijana mmoja ambaye anaonekana yupo katika hali ya kutojifahamu ambaye anadhaniwa kuwa ni XXXTentacion akiwa ameketi katika siti ya dereva ya gari yake. 


XXXTentacion aliweza kupata umaarufu kupitia mtandao wa SoundCloud na kufanikiwa kutoa album yake ya kwanza iliyojulikana kama 17" mwaka jana. Album yake ya pili "?" iliweza kushika namba 1 katika chati za mwezi March 2018. 

XXXTentacion pia amekuwa akihusishwa na kuwa na bifu kati ya wasanii wenzake wakiwemo Drake, na member wa kundi la Migos maarufu kama Offset ambao hawajazungumzia chochote mpaka sasa kuhusiana na kifo cha msanii huyo.

Moja kati ya video za mwisho kabisa za msanii huyo, ilimuonesha akiwa kwenye gari akijirekodi akisema kuwa "Endapo itatokea siku moja nimekufa ghafla kabla ya kuishi ndoto zangu, nataka nigakikishe kuwa watu wengi wanapata majibu ya maswali wanayojiuliza kuhusu mimi kupitia muziki wangu, na nataka nihakikishe kuwa angalau watoto takribani milioni 5 wanakuwa na furaha kupitia maisha yangu.
Baadhi ya wasanii wameonekana kutoa pole kwa familia ya msanii huyo na kuelezea walivyoumizwa na kifo chake katika mitandao ya kijamii hususani Twitter. 




No comments