Breaking News

England, Sweden na Belgium zaanza vyema mechi zao za ufunguzi Kombe la Dunia

Kombe la Dunia nchini Urusi liliendelea hapo jana na Sweden waliweza kuanza vyema mchezo wao wa kwanza baada ya kupata ushindi mbele ya South Korea kwa mkwaju wa penati dakika ya 65 bao lililofungwa na Andreas Granqvist.
Mchezo wa kwanza wa kundi G nao ulipigwa hapo jana, Belgium wakapata ushindi mnono mbele ya Panama kwa kupata mabao matatu, mabao ambayo yalifungwa na Dries Mertens dakika ya 47' na Romelu Lukaku dakika ya 67' na 75 akipewa assist na Kevin De Bruyne na Eden Hazard. 

Mchezo wa pili wa kundi G nao pia ulipigwa hapo jana, wakati England walipoumana na Tunisia, mchezo ambao uliondoa matumaini kwa waafrika wengi bado ya kuona timu nyingine ya afrika ikipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye mashindano hayo.

England walianza kupata goli kupitia kwa nahodha wao Harry Kane dakika ya 11 ya mchezo kupitia kwa mkwaju wa kona, huku Tunisia wakipata bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 35 kupitia kwa Ferjan Sassi. England walipata bao lao la pili kupitia tena kwa Harry Kane dakika za nyongeza (90 + 1) na kufanya mchezo huo kumalizika kwa England kupata ushindi wa 2 - 1. 

Kundi G sasa litakuwa linaongozwa na Belgium wenye point 3 na magoli 3, wakifuatiwa na England wenye point 3 na tofauti ya bao moja. Halafu Tunisia na Panama wakiwa wanashika mkia wote wakiwa hawana point. 

No comments