Breaking News

Samsung yatarajia kuja na Galaxy S10


Kampuni ya Samsung kupitia simu zake za toleo la "S" inakaribia kutimiza miaka 10 hivi karibuni, na kampuni hiyo imesema kuwa inatarajia kufanya mabadiliko makubwa sana ili kuweza kusherehekea sherehe hiyo kwa uzuri zaidi. Kutoka kwa wafanyakazi wa ndani wa branch ya kampuni hiyo ya Korea Kusini, Galaxy S10 itakuja katika matoleo matatu tofauti. 

Simu zote hizo katika matoleo hayo matatu, zitakuja na utofauti wa idadi ya Camera, huku toleo kubwa kabisa likitarajiwa kuja na idadi ya camera tatu upande wa nyuma na fingerprint scanner ambayo itakuwa ndani ya camera. Yaani mtu mwingine yeyote hataweza kupiga picha bila ya kuwa na ridhaa ya mwenye simu maana lazima aweke fingerprint yake. 

Simu zote hizo tatu tayari zimeshaanza kutengenezwa na code ya simu hizo itaitwa "Beyond". Beyond 0, itakuja na camera moja upande wa nyuma na screen yenye 5.8 inches lakini pia haitakuwa na edge. Beyond 1, itakuja na kioo chenye size ileile kama Beyond 0, lakini yenyewe itakuwa na edge lakini pia itakuja na camera mbili upande wa nyuma. 


Beyond 2 ndiyo ambayo inatazamiwa kuwa balaa zaidi, kwasababu itakuja na camera tatu upande wa nyuma, ikiwa na fingerprint kwenye camera pia. Ingawa idea hii tayari ilishaanza kutumika kwenye Huawei, Samsung wapenga kuiongezea ujuzi na kuweka utafauti na ule uliokuwepo kwenye Huawei P20 Pro.

Namna simu hizi na matoleo haya ya Samsung yatakavyotoka, yatatukumbusha kipindi Samsung wametoa S6, ambayo haikuja na note yake, isipokuwa ilikuja na simu ya kawaida ya Galaxy S6, wakatoa na Galaxy S6 Edge wakamaliza na Galaxy S6 Edge+. Ubadilishaji huu wa namna ya utoaji wa kila siku unaweza ukawa umetokana na manunuzi madogo katika masoko yao makubwa yakiwemo China na India pamoja na watumiaji wengine wote duniani katika mwaka 2017.

No comments