Senegal yarejesha matumaini ya waafrika. Misri Hoi
Jana huko nchini Urusi kwenye mashindano ambayo yanaendelea ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Senegal iliweza kurudisha matumaini kwa mataifa ya Afrika baada ya kuwafunga Poland kwa mabao 2 - 1 ikiwa ndio timu pekee kutokea Afrika kupata ushindi tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Senegal iliweza kupata goli lao la kwanza kupitia kwa Thiago Cionek aliyejifunga baada ya kupigwa shuti kali na mchezaji wa Senegal akiwa na nia ya kuokoa. Goli la pili lilifungwa na Mbaye Niang dakika ya 60 ya mchezo huo kisha Poland wakapata bao dakika za mwishoni kwa kichwa kwa mchezaji wao Krychowiak dakika ya 86.
Mchezo mwingine ulikuwa wa Japan dhidi ya Colombia. Japan waliweza kushinda mchezo huo kwa kupata penati mnamo dakika ya 6, penati iliyofungwa na Shinji Kagawa kisha Colombia wakapata bao lao kupitia kwa Juan Quintero dakika ya 39 na Japan wakaongeza bao la pili kupitia kwa Yuya Osako dakika ya 73 kabla ya mchezo huo kuisha.
Mchezo wa tatu ikiwa ni mzunguko wa pili wa kundi A, Urusi waliweza kupoteza matumaini ya Misri baada ya kuwashinda kwa mabao 3 - 1. Mabao hayo yalifungwa na Ahmed Fathi aliyejifunga dakika ya 47, Denis Cheryshev akaiandikia Urusi bao la pili dakika ya 59, huku Artem Dzyuba akiongeza bao la tatu dakika ya 62. Mohammed Salah aliweza kutafuta penati dakika ya 73 na kushinda bao la kufuta machozi.
Michezo mingine itapigwa hapo leo mnamo saa 9 ambapo Portugal wakiongozwa na staa wao Cristiano Ronaldo watawavaa Morocco, huku Uruguay ikiminyana nguvu na Saudi Arabia saa 12 jioni, na Spain kutoana jasho na Iran saa 3 usiku.
No comments