Breaking News

Tetesi za Soka barani Ulaya 19.06.2018 Jumanne

Arsenal wanakaribia kuwasaini kwa pauni milioni 48 kipa wa Bayer Leverkusen mjerumani Bernd Leno, 26, na kiungo wa kati wa Sampdoria raia wa Uruguay Lucas Torreira. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard ametoa onyo kwa Chelsea, huku mchezaji huyo wa miaka 27 akikiri kuwa Real Madrid huenda wakamtafuta. (Sun)
Aliyekuwa kocha na Napoli Maurizio Sarri na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Gianfranco Zola atathibitishwa kama mmoja wa mameneja wa Chlesea wiki hii ikiwa makubaliano yataafikiwa kusitisha mkataba wa kocha wa sasa Antonio Conte
Everton wanataka wing'a wa Sporting Lisbon raia wa Ureno Gelson Martins, 23, pamoja na mlinzi wa Ajax raia wa Uholanzi Matthijs De Ligt. (Telegraph)
Mkurugenzi mpya wa kandanda wa Everton Marcel Brands yuko huru kuvamia klabu yake ya zamani PSV Eidhoven, kumsaini wing'a Hirving Lozani, 22, ambaye alifunga bao la ushindi dhidi ya Ujerumani mechi ya Kombe la Dunia, (Echo)
Manchester City wanakaribia kuafikia makubaliano ya pauni milioni 46.5 kwa kiungo wa kati wa Napoli Muitalia Jorginho, 26. (Sky Sports)
Kipa wa Manchester United David de Gea huenda akawa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani wakati raia huyo wa Uhispania, 27, atasainia mkataba mpya. (Marca)
Newcastle United wamewaambia Feyenoord kuwa watahitajika kulipa paunia milioni 20 kumsaini mshambuliaji raia wa Denmark Nicolai Jorgensen 27. (Chronicle)
Liverpool wataka pauni milioni 15 kwa Daniel Sturridge, huku Sevillah ikifufua matumaini kwa mshambuliaji huyo wa England na Fernerbahce wakimwinda mchezaji huyo wa miaka 28. (Telegraph)
Wachezaji wa Ubelgiji Toby Alderweireld na Mousa Dembele, pamoja na wa Chelsea Thibaut Courtois na Eden Hazard, wameamua kungoja hadi kukamilika Kombe la Dunia ili kutatua hatma yao kwenye vilabu. (Evening Standard)
Mbio za Watford za kumwinda kipa hazionekani kutulia baada ya kuhusishwa na kumtafuta mchezaji raia wa Ureno wa kikosi kisichozidi miaka 23 Bruno Varela. (Watford Observer)
Nottingham Forest bado wanataka kumrejesha mshambuliaji wa Cardiff City Lee Tomlin lakini fursa nzuri kwao ni kufanya hivyo kwa mkopo kwa raia huyo wa England mwenye miaka 29. (Nottingham Post)
Leeds United wametangaza ofa kwa mchezaji wa Birmingham City, David Stockdale lakini hawatimizi thamani iliyotangazwa na mahasimu kwa kipa huyo wa England, (Birmingham Mail)
Gavin Reilly, 25, ametangzza kuondoka kwake huko St Mirren huku Sunderland wakitarajiwa kumchukua kiungo huyo wa kati wa Stolland. (Chronicle)

No comments