Breaking News

Zari sio chanzo cha msanii Diamond Platnumz kukonda, meneja wake asema

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa WCB amekuwa kwenye headlines sana na moja kati ya vitu vinavyo trend ni mwili wake kuisha.

Baada ya Diamond kuonekana anapungua mwili kwa kasi habari zilisambaa Mtandaoni kuwa kisa ni Zari ambapo ilidaiwa baada ya kumwagwa na Zari Diamond alipata mawazo sana na hata kudaiwa eti sahivi hapati matunzo aliyokuwa anapata wakati yupo na Zari.

Lakini Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni kukosa muda wa kulala kutokana na jukumu zito la ujio wa Wasafi TV.

"Kuna baadhi ya watu wanasema msanii wangu anapungua mimi na nenepa navimba, Kama hamjui Media sio kitu kidogo, wakati tunaanza tulijua ni kazi ndogo, kwa miezi sita non stop msanii wangu analala masaa mawili tu, kwa sababu ya kuandaa hiki mnachokiona machoni mwenu.. Wiki mbili za mwanzo tukawa tunakasirika kwa nini anafanya kazi ngumu, ilipofika mwezi tukawa tunaona  ana-loose weight (kupungua uzito) na bado kazi zinaendelea tukawa tunashangaa ana nia gani huyu".

Lakini pia mwana Familia wa Diamond mwenyewe,ambaye ni dada yake Esma aliwahi kunukuliwa akisema kaka yake kapungua kwa kumiss penzi la Zari.
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa WCB amekuwa kwenye headlines sana na moja kati ya vitu vinavyo trend ni mwili wake kuisha. Baada ya Diamond kuonekana anapungua mwili kwa kasi habari zilisambaa Mtandaoni kuwa kisa ni Zari ambapo ilidaiwa baada ya kumwagwa na Zari Diamond alipata mawazo sana na hata kudaiwa eti sahivi hapati matunzo aliyokuwa anapata wakati yupo na Zari. Loading... Lakini Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni......

No comments