Breaking News

Putin: Makundi nchini Marekani yanaharibu mafanikio yetu na Trump

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameyashutumu baadhi ya makundi ndani ya Marekani kwa kujaribu kudhoofisha mafanikio ya mkutano wake wa kwanza wa kilele na rais Donald Trump, lakini amesema viongozi hao wawili hata hivyo tayari walikwishaanza kuboresha mahusiano kati ya nchi zao. 


Putin na Trump walikutana kwenye mkutano huo wa kwanza wa kilele mjini Helsinki Jumatatu hii, tukio lililoibua ukosoaji mkubwa nchini Marekani, baada ya Trump kukataa kumlaumu Putin kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016, ingawa Putin mwenyewe anakana. 

Akizungumza na wanadiplomasia kutoka maeneo mbalimbali duniani waliokutana mjini Moscow, Putin amesema mkutano wake na Trump wa Helsinki ulikuwa wa mafaniko makubwa, ingawa watu wenye nia mbaya nchini humo wanajaribu kuyahujumu mafanikio yake kwa kuyaharibu mahusiano ya mataifa hayo kwa ajili ya matakwa yao katika mapambano ya kisiasa ya ndani ya Marekani.

No comments