Breaking News

Koulibaly awataka Napoli kushinda kombe la Europa

Beki wa Kati wa klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly amelalamika kuhusu timu yake kupoteza mchezo wao wa kombe la mabingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Liverpool lakini anaamini kuwa wataweza kushinda kombe la Europa.


Klabu hiyo kutoka nchini Italia, iliweza kumaliza michezo yao ya kundi C ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya kupigwa kichapo cha 1 - 0 na klabu ya Liverpool katika uwanja wa Anfield siku ya Jumanne.

"Tunaomba radhi sana kwa mashabiki wetu kwani tulikuwa na malengo ya kuchukua kombe hili msimu huu lakini haikuweza kwenda sawasawa na malengo tuliyojiwekea. Hivyo tunaomba radhi sana sana" yalikuwa ni maneno ya beki huyo wa Napoli.




No comments