Breaking News

Kuondoka kwa Rich Mavoko kwenye label ya WCB; Faini, BASATA, Diamond

Msanii aliyekuwa amesainiwa kwenye label ya Wasafi maarufu kama Rich Mavoko inasemekana kuwa hakulipa pesa yake kwa ajili ya kuvunja mkataba wake na kuondoka kwenye label hiyo.

Dada yake, Wenceslaus Dokii, alisema kuwa Diamond Platnumz alimtaka Rich Mavoko alipe Tsh. Milioni 500 kwa ajili ya kuvunja mkataba wake jambo ambalo Rich Mavoko hakukubaliana nalo.

Kuondoka kwa Rich Mavoko katika label ya WCB hakukuwa kwa namna nzuri, Rich alieleza kuwa mkataba wake katika label hiyo haukuwa mzuri na ulikuwa ni wa unyonyaji.

“Walituambia tuwalipe pesa mob, nikamwambia Diamond, no we can’t pay you. It was millions of money inalingana kama ya Harmonize. Nilimwambia pia Sallam (Diamond’s manager), you guys nendeni mkajipekue mjitazame tena, hicho kitu mnachokitaka, is it fair?” Hayo yalikuwa maneno ya Dokii aliyoyaongea kwenye interview hivi karibuni."

Harmonize ambae pia alikuwa moja kati ya wasanii waliosainiwa WCB, wakati alipotaka kuondoka katika label hiyo, aliambiwa alipe kiasi cha pesa kinachofanana na hicho, jambo ambalo lilimbidi auze nyumba zake tatu na moja ya viwanja vyake ili kuongeza pesa. Pesa hiyo ambayo ilibidi alipe, ilikuwa inamfanya kumpa haki zote na umiliki kuhusiana na nyimbo zake alizofanya wakati yupo WCB.

Kwa upande wa Rich Mavoko, mambo hayakwenda sawa, na mgogoro ulikuwa mkubwa, jambo lililopelekea malalamiko hayo kwenda kwenye Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na huko ndiko suluhisho lilipatikana. Rich Mavoko aliondoka kwenye label hiyo pasipo kulipa pesa yoyote. Jambo ambalo bado halijawekwa wazi mpaka hivi sasa ni kama je msanii huyo bado ni ana haki zote za umiliki wa nyimbo zake au la.

Mavoko aliondoka WCB mwaka 2018, ikiwa ni miaka miwili tu tangu kuvunja mkataba wake na King Kaka Record Label, Kaka Empire mnamo 2016.

No comments