UN: Athari za corona kusababisha vifo 51,000 vya watoto MENA
Mashirika ya Umoja wa Matifa yameonya leo hii, kwamba hadi mwishoni wa mwaka janga la virusi vya corona linaweza kusababaisha vifo vya nyongeza ya watoto 51,000 walio chini ya miaka mitano, katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, yamesema usumbufu wa huduma muhimu za kiafya na lishe unaotokana na janga hilo, unahatarisha kurudisha nyuma maendeleo ya watoto kwa karibu miongo miwili katika maeneo hayo.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa huko mjini Amman, Jordan, mashirika hayo yamezisihi serikali kufanya kazi ya kuongeza uaminifu katika mifumo ya afya ya umma, na kukuza tabia zinazofaa za utunzaji kati ya familia
No comments