Breaking News

Maandamano kulaani kifo cha Floyd yaendelea Marekani


Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza kwenye miji mbalimbali nchini Marekani katika siku ya 12 ya maandamnao makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa dhidi ya ukatili wa polisi yaliyochochewa na kifo cha mmarekani mweusi George Floyd. Katika miji ya Philadelphia, New York, Atlanta, Los Angeles, San Diego, Seattle na miji mingine mikubwa waandamanaji walimiminika mitaani kudai haki kwa wote waliohusika na kifo cha Floyd.

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika pia mbele ya ikulu ya Marekani wakipaza sauti ya kutaka kuthaminiwa kwa maisha ya watu weusi huku wengine wakitoa wito wa kupunguzwa bajeti ya polisi ili kuwasaidia wenye mahitaji. Mji mkuu Washington umekuwa kitovu cha maandamano na kwa sehemu fulani hasira zinaelekezwa kwa rais Donald Trump ambaye amechua msimamo mkali dhidi ya waandamanaji ikiwa ni pamoja na kutishia kutumia jeshi kuwatawanya.

No comments