Idadi ya vifo vya COVID-19 yakaribia 400,000 duniani kote
Idadi ya waliokufa kutokana na COVID -19 duniani imekaribia watu 400,000 leo huku vifo vikiongezeka kwenye mataifa ya Amerika ya Kusini. Hivi sasa Brazil ni nchi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo duniani huku rais Jair Bolsonaro wa nchi hiyo akitishia kuiondoa nchi yake kutoka kwenye shirika la Afya duniani WHO kwa madai ya upendeleo. Nchini China serikali imeripoti kuanguka kwa mauzo ya nje kufuatia kupungua kwa mahitaji na kudhoofika kwa nguvu ya uchumi kwenye mataifa mengi duniani.
Hayo yanajiri wakati mataifa ya Ulaya yaliyoathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona yanajaribu kufufua tena shughuli muhimu za utalii wakati huu wa majira ya kiangazi. Umoja wa Ulaya umesema utafungua mipaka yake kwa wasafiri kutoka nje ya kanda hiyo mapema mwezi Julai baada ya mataifa kadhaa ya umoja huo kuanza kuruhusu wageni kutoka mataifa jirani ya Ulaya kuyatembelea.
No comments