Maelfu wajitokeza wakiwemo wasanii na watu mashuhuri kuuaga mwili wa George Floyd
Watu mashuhuri, wanamuziki na viongozi wa kisiasa nchini Marekani walikusanyika mbele ya jeneza la George Floyd, katika ibada ya misa iliyojaa mihemko kumuaga Floyd ambaye kifo chake kimesababisha maandamano kote duniani.
Ibada hiyo ya kumuaga George Floyd ambayo ni ya kwanza kufanyika katika miji mitatu tofauti ndani ya siku sita, iliyoanzia mjini Minneapolis, katika eneo takatifu kwenye chuo kikuu cha North Central huku jaji mmoja katika eneo karibu na hilo akitoa dhamana ya dola 750,000 kwa kila mmoja ya maafisa watatu wa polisi walioshitakiwa kwa kushiriki katika mauaji ya George Floyd
No comments