Ligi ya Mabingwa barani Ulaya leo 26.02.2020 Real Madrid Vs Man City, Lyon Vs Juventus
Ligi ya Mabingwa barani Ukaya iliendelea tena hapo jana pale ambapo Napoli waliwakaribisha mabingwa wa Hispania Barcelona katika hatua ya mtoano (Knockout Stage). Mechi hiyo ambayo iliangaliwa na watu wengi, iliwashuhudia wawili hao wakitoka sare ya 1-1 mabao hayo yakifungwa na Mertens kutoka Napoli na Antoinne Griezmann kutoka Barcelona.
Chelsea nao walishuka dimbani Stamford Bridge wakiwakaribisha mabingwa wa Ujerumani Bayern Munchen na mechi hiyo ilimalizika kwa Bayern kupata mabao matatu kwa bila, mabao ambayo yalifungwa na Gnabry katika dakika ya 51 na 54 na bao la mwisho likifungwa na Robert Lewandowski 76.
Leo ligi hiyo ya mabingwa itaendelea tena na Real Madrid watakuwa nyumbani wakiwakaribisha Manchester City huku Lyon wao wakiwakaribisha Juventus.
Madrid watashuka dimbani leo huku wakiwakosa baadhi ya wachezaji wake kama Eden Hazard, Luka Jovic na Marco Asensio, huku Man City ikiwakosa Leroy Sane na Raheem Sterling.
Rekodi:
Man City imeshawahi kukutana na Real Madrid mara nne kwenye mashindano haya, na Man City hajawahi kuibuka mshindi katika mechi zote nne, wamefungwa mara mbili, wametoka sare sara mbili.
Juventus nao wakiongozwa na Cristiano Ronaldo, wanatarajia kuendeleza ubabe wao kwenye mashindano hayo, huku ikizingatiwa kwamba tangu mwaka 2010 kwenye mashindano hayo, Lyon wamekutana na Juve mara 5 huku Juventus ikishinda mara 4 na kutoka sare sara 1.
Nini maoni yako kuhusu mechi za leo, tuandikie kupitia sehemu ya comment iliyoko hapo chini
No comments