Breaking News

Nchi 7 zawania viti vitano vya Baraza la Usalama la UN


Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litawachagua leo wanachama watano wapya wa Baraza la Usalama kwa mwaka wa 2021 na 2022, huku mapambano yakiwa kwenye viti vya nchi za Magharibi na Afrika. Kenya na Djibouti zinawania kiti kimoja, wakati katika upande wa magharibi, mataifa matatu Canada, Ireland na Norway yanagombea viti viwili miongoni mwao.

Kenya ina uungwaji mkono wa Umoja wa Afrika, lakini Djibouti inasema inapaswa kupata kiti hicho kwa sababu Kenya ilishawahi kushiriki kwenye Baraza la Usalama katika miaka ya nyuma pamoja na kanuni ya kupokezana. Mataifa yote mawili yanaangazia majukumu yao ya kusaka amani katika eneo la Pembe ya Afrika, pamoja na michango yao katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Katika eneo la Asia Pasifiki, India, ambayo imekuwa ikijaribu bila mafanikio kushinda kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama lililotanuliwa, imejihakikishia kiti kwa sababu inagombea bila kupingwa, kama tu ilivyo kwa Mexico katika eneo la Amerika Kusini na Carribbean.

No comments