Breaking News

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yasaini mkataba wa kuagiza chanjo ya corona

Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uholanzi zimesaini mkataba wa kuagiza jumla ya dozi milioni 300 za chanjo ya virusi vya corona ambayo hivi sasa inaendelea kufanyiwa utafiti. Wizara ya afya ya Ujerumani ilisema jana kuwa nchi hizo nne zimesaini mkataba wa awali na kampuni ya Famasia ya AstraZanecca na kwamba zimo katika mazungumzo na makampuni mengine ya famasia kuhusiana na chanjo za COVID-19.

Aidha wizara ya afya iliongeza kuwa pindi chanjo hiyo itakapokamilika itasambazwa katika mataifa hayo manne na kuongeza kwamba nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaweza kushiriki kwenye programu. Chanjo hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. Shirika la afya duniani WHO, lilisema chanjo kutoka kampuni ya AstraZeneca, inayofanyiwa utafiti na chuo kikuu cha Oxford ni moja ya chanjo chache ambazo kwa hivi sasa ziko katika hatua ya tathmini.

No comments