China yaripoti maambukizi mapya 54 ya virusi vya corona
China leo imeripoti maambukizi mapya 54 ya virusi vya corona, ikiwa ni kiwango cha juu katika takwimu zinazotolewa kila siku tangu mwezi wa nne, wakati ambapo wasiwasi ukizidi kuongezeka juu ya kurejea tena kwa maradhi hayo. Tume ya taifa ya afya imesema maambukizi 36 kati ya hayo yote ni ya ndani katika mji wa Beijing.
Matukio hayo yamesababisha kuwekwa hatua za karantini katika baadhi ya vitongoji. Wakati huo huo takwimu za chuo kikuu cha John Hopkins zinaonyesha kuwa, Marekani imeorodhesha vifo vingine 734 ndani ya saa 24 zilizopita vinavyohusiana na virusi vya corona na kuifanya idadi jumla kufikia 115,347. Marekani ndio taifa lililoathiriwa zaidi na virusi hivyo na inaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha vifo na pia maambukizi. Kwa siku, Marekani inathibitisha maambukizi mapya karibu 20,000 ya virusi vya corona
No comments