Breaking News

Wachina wanaoishi jijini Nairobi waomba kurudishwa kwao kutokana na maambukizi ya corona nchini Kenya

Idadi ya wananchi wa kichina zaidi ya 400 wanajiandaa kuondoka nchini Kenya wiki hii kwa hofu ya virusi vya corona. 

Wananchi hao walipokea tamko kutoka katika mahakama kuu nchini humo, tamko lililotaka serikali iwaachie wananchi hao kurudi nchini kwao ifikapo tarehe 16 Juni sababu serikali ya nchini humo haina uwezo mkubwa wa kutibu na kuhimili au kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Justice Weldon Korir ambae ndiye aliyetoa tamko hilo alisema kuwa wananchi hao wapewe ruhusa na ndege ziwachukue ziwarudishe nchini kwao akielezea kuwa miundombinu ya afya nchini humo haina uwezo wa kuhimili idadi ya watu wengi kadri inavyozidi kuongezeka.

Bwana Isaac Okinyo ambae ni mwanasheria, alieleza kuwa kwa sasa kila jambo liko tayari kwa ajili ya kuwasafirisha wananchi hao, na hivyo kwa sasa wanasubiri tu ruhusa kutoka katika wizara ya mambo ya nje ya nchini humo. Aidha mwanasheria huyo alisema kuwa wananchi hao wanasema kuwa China kuna mahali salama zaidi na vifaa vyenye teknolojia kubwa ya kuweza kuwakinga na maradhi hayo.

"Wachina wengi wanahofu wakiwa nchini hapa, wengine hawaoni usalama tu, hivyo ni bora warejee nchini kwao. Vituo vyote vya kujitenga vimejaa na hata vifaa havitoshi kwa ajili ya kupimia havitoshi, hivyo acha tu warudi kama ambavyo wanahitaji"

Wananchi hao ambao wanatarajiwa kuondoka hivi karibuni wataongozwa na balozi wa china nchini Kenya Wu Peng.
Chini ndiyo ilikuwa sehemu ambapo homa hiyo ya mapafu ilianzia, mnamo December 2019 huko Wuhan, mji ambao unakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 11.

Ugonjwa huo ambao ulianza kama moja ya maradhi ya kuenea, hivi sasa umekuwa jambo la kuumiza kichwa duniani kote, ukiwaathiri watu zaidi ya milioni 7 na kuua watu 406,000 takwimu hizo ikiwa ni kutoka katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ambacho kinakusanya data hizo kutoka katika vituo vya afya vya kitaifa na kimataifa.

Tangu hapo ugonjwa huo umeenea katika nchi zaidi ya 200 duniani kote huku Marekani, Brazil, Russia, zikiwa zimeathirika sana na ugonjwa huo zikifuatiwa na Uingereza, Hispania pamoja na Italy. Kenya imetangaza kuwa na kesi 3,305 mpaka kufikia ijumaa na idadi ya vifo ikiwa ni 96.

No comments