Breaking News

Bolt: Nitaishabikia Argentina Kombe la Dunia

Usain Bolt tayari ameshashinda tuzo mbalimbali zikiwemo tuzo za dhahabu za Olympic lakini baada ya timu yake ya taifa kushindwa kufuzu kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia, Bolt aliibuka na timu mpya ya kuishangilia katika mashindano hayo.

Bolt ndiye mwanariadha bora kabisa katika kizazi chake akiwa tayari ameshashinda tuzo za mita 100 na mita 200 mara tatu mfululizo kati ya mwaka 2008 hadi 2016.
Lakini raia huyo wa Jamaica pia ni mshabiki na mpenzi wa mpira wa miguu. Na aliweka wazi ni timu gani ambayo ataishabikia katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Russia. 

"Kwangu mimi nitashabikia Argentina. Nadhani tuna nafasi nzuri ya kushinda na kama tutaweza kucheza vizuri katika makundi basi nadhani tutakuwa tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mitoano, na huenda mpaka robo fainali, nusu fainali hata fainali" alisema Bolt

Argentina waliweza kufuzu kucheza katika mashindano hayo baada ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Ecuador na shukrani kwa Lionel Messi baada ya kushinda hat trick iliyosaidia kuipeleka timu hiyo nchini Urusi.

No comments