Breaking News

Messi aionya Argentina kuhusu Nigeria

Ingawa Argentina wameshinda mechi zao zote katika mashindano yaliyopita, Messi amewaonya wachezaji wenzake kuwa Nigeria sio timu ya kuichukulia poa. 

Argentina wameweza kuwashinda Nigeria katika mashindano yote yaliyopita waliyokutana lakini hivi karibuni mwezi Novemba, Argentina walipoteza kwa mabao 4 - 2 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa kirafiki. 

Wawili hao watakutana tena katika mechi ya mwisho ya makundi baada ya wao wote kukutana na Iceland pamoja na Croatia katika kundi D na Messi amesema anadhami mechi hiyo itakuwa ngumu sana.

Hatufahamu mengi kuhusu Nigeria lakini timu za kiafrika mara nyingi zimekuwa ni ngumu, na huwa zinacheza kwa nguvu kwa hivyo tutegemee mchezo mgumu.

No comments