Cardi B na Offset waeleza story yao ya mapenzi kwenye jarida la "RollingStone"
Wakiwa wanatazamia kupata mtoto wao wa kwanza, Cardi B na Offset wamefunguka kuhusu mahusiano yao, yalikuwaje na yalitokeaje pamoja na mtoto anayetarajiwa kuja hivi karibuni kwenye jarida la RollingStone. Mwandishi Vanessa Grigoriados alisafiri mpaka wanapokaa wapenzi hao kuzungumza nao juu ya ukurasa mwingine wa maisha wanaotarajia kuuanza.
Katika mahojiano, Cardi B alielezea anachokumbuka siku aliyogundua kuwa ni mjamzito. Anasema kuwa baada ya kujipima na kifaa maalumu na kugundua kuwa ni mjamzito, haraka sana alimpigia simu mpenzi wake "Offset" kwenye mtandao wa FaceTime na kumweleza juu ya jambo hilo. Mpenzi wake alionekana kufurahishwa sana na jambo hilo kiasi cha kubaki akiwa anatabasamu tu.
Wakati Offset akiwa anamtaka mpenzi wake Cardi B aulinde na kuulea ujauzito huo, baadhi ya rafiki zake Cardi walikuwa wakimshauri kuwa autoe wakiwa wanadhani kuwa utaharibu kazi yake ya muziki.
Cardi ataanza tour yake na Bruno Mars mwezi Septemba, hali ya kuwa na ratiba ngumu sana ya kuwa na mwanae. "Sitaki kukosekana hata kwa sekunde moja, alisema. Sitaki kukosa tabasamu lake, sitaki kukosa mara yake ya kwanza akiwa anatembea, sitaki mwanangu aje kutojua kunitofautisha kati yangu mimi mama yake na mlezi wake(babysitter)
Katika hali ya kuongeza familia yake, Offset anatarajia kuja kivingine kuhusiana na suala la muziki. Anapanga kutoa nyimbi nyingi akiwa ameimba peke yake, sio kama ambavyo tumekuwa tukimzoea na kundi lake la Migos. Tayari ana collaboration na 21 Savage na Metro Booming ambazo zinatarajiwa kutoka hivi karibuni.
No comments