Crespo: Messi anahitaji msaada kushinda Kombe la Dunia
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina amemkingia kifua Staa wa timu hiyo Lionel Messi na kusema kuwa anahitaji msaada kutoka kwa wachezaji wenzake kama watahitaji ashinde Kombe hilo.
Staa huyo wa klabu ya Barcelona alishindwa kuiongoza timu yake ya taifa kupata ushindi dhidi ya Iceland siku ya Jumamosi kwenye ufunguzi wa mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia, mechi ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya 1 - 1.
Crespo ambaye ameichezea Argentina mechi 64 alisema kuwa wachezaji wenzake watahitaji kumsaidia mchezaji huyo kwa sana kama wana nia moja ya kutwaa Kombe hilo.
Crespo alisema kuwa "Kwanza Messi alicheza vizuri sana katika mechi hiyo hilo halina ubishi. Lakini yeye sio Maradona na watu wasimfananishe na mchezaji huyo. Hilo linapaswa lieleweke kwa mashabiki lakini pia hata kwa wachezaji wenzake. Anacheza vizuri Barcelona kwa sababu anapata msaada wa kutosha lakini sio hivyo kwa upande wa Argentina.
Argentina wataingia tena kucheza na Croatia katika mechi yao ya pili ya Group D siku ya Alhamisi. Ikumbukwe kuwa Croatia waliwafunga Nigeria kwa mabao 2 - 0 siku ya Jumamosi.
No comments