Harry Kane: Kuwa Captain hakubadilishi hali yangu ya mchezo
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane anaamini kwamba kuwa Captain hakutabadilisha mchezo wake atakapowaongoza Uingereza kucheza dhidi ya Tunisia katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi G.
Harry Kane alifunga magoli matano katika mechi za kufuzu kucheza mashindano hayo na ameweza kushinda magoli 30 katika ligi kuu ya Uingereza.
"Kwangu mimi hakuna kitu kinachobadilika, ninapokuwa Captain au nisipokuwa. Siku zote nimekuwa nikifanya yale ambayo timu yangu inahitaji wa wakati husika na kuhakikisha kuwa tunapata ushindi, na mara tumekuwa tunafanikiwa.
"Wachezaji wanaifahamu timu na wanajua majukumu yao na hilo linasaidia sana. Tunasonga mbele kama kitu kimoja na tunashirikiana" alisema Harry Kane.
No comments