Breaking News

Drake atarajia kumchana Kanye West kwenye album yake mpya


Tuna wiki moja tu kusikia albamu ya Drake ambayo kutarajiwa sana, lakini kumekuwa na maneno mengi yanayoendelea kuongelewa. Mashabiki wamekuwa wakiuliza kama Drizzy atamjibu Pusha T baada ya kupata disstrack ya mwisho ya "Story of Adidon". DJ Akademiks alizungumza na Drake na ndipo Drizzy alimwambia kwamba hana sababu ya kufikiria sana kwasababu baada ya kutoa album hiyo mashabiki zake wote wataweza kupata majibu yote ya kile ambacho wanakiulizia hivi sasa. 

Aidha, Inaonekana kama Drake amekuja na kitu kingine pia kwa ajili ya Kanye West. Katika usiku wa kuamkia Jumamosi, kampuni ya Apple kupitia Apple Music iliweza kutweet mstari uliosomeka kuwa "Fashion Week is more your thing than mine" ukiwa umemtag Drake na album yake ya Scorpion. Ni wazi kuwa mashabiki wanadhani kuwa huu mstari umekuwa "dedicated" kwa Kanye West.

Lakini sasa inapaswa tusubiri album na kusikiliza kwa umakini katika nyimbo hii na kugundua kuwa Drake alikuwa anamuongelea kweli Kanye West au sivyo, lakini katika hali ya kawaida tunafahamu ni jinsi gani Kanye West anapenda sana kufanya show zake za mambo ya Fashion.

Kumekuwa na tetesi nyingi zaidi pia kuwa huenda album hii ikawa na nyimbo nyingi sana kiasi cha kuwekewa pande mbili yaani Side A na Side B ili aweze kuelezea kiumakini zaidi hali yake ya maisha kwa sasa.

Unaweza kuangalia hiyo tweet ya Apple Music Hapa:


No comments