Wahamiaji watano wafariki na wengine 200 waokolewa Libya
Wahamiaji Ä·Ä· wamefariki dunia na wengine karibu 200 kuokolewa pwani ya Libya, wakati walipojaribu kuvuka bahari ya Mediterenia kuingia Ulaya katika maboti mawili.
Watoto watatu na wanawake tisa ni miongoni mwa wahamiaji 94 waliokolewa jana Ijumaa wakati boti lao lilipozama maili chache mashariki mwa mji wa Tripoli. Wahamiaji watano kutoka Sudan, Nigeria,
ĶChad na Misri waliokuwamo katika boti hiyo walipoteza maisha. Wengine 91 waliokuwa wakisafiri katika boti nyingine waliokolewa katika eneo hilo hilo, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la majini la Libya, Ayoub Kacern.
Jumla ya wahamiaji 900 wameokolewa au kuzuiliwa na jeshi hilo la Libya tangu Jumatano, mnamo ambapo safari zikipamba moto kwasababu ya hali nzuri ya hewa. Libya ni njia kuu ya safari ya maelefu ya wahamiaji walio na matumaini ya kufika Ulaya, ingawa mamia yao huzama kila mwaka katika jitihada hizo.
No comments