Drake aweka rasmi siku ya uzinduzi wa album yake
Album mpya ya Drake kwa sasa inataarifa rasmi kuhusu kutambulishwa kwake. Baada ya miezi miwili tangu atambulishe jina halisi la Album hiyo ambayo inajulikana kama "Scorpion" Drake sasa ametangaza rasmi ujio wa album hiyo kwamba itakuwa ni June 29.
Msanii huyo wa miondoko ya rap kutokea Toronto Canada mnamo June 13 alitumia ukurasa wake wa Instagram kuweka rasmi tarehe na artwork ya album hiyo. Cover hiyo ilikuwa inamuonesha rapper huyo katika picha ya black & white na sahihi(signature) yake pia ambayo alikuwa imepigwa kwenye picha hiyo.
Album hiyo itawasili muda muafaka kabisa wakati "Aubrey(Drake) and The Three Migos Tour" ya msanii huyo itakuwa ikianza July 26 katika mji wa Salt Lake. Rapper huyo ataungana na wasanii wenzake maarufu kama Migos na kufanya ziara hiyo katika miji kama vile Denver, Toronto, Detroit, Chicago, New York, Boston, Miami, Houston na mingine mingi.
Unaweza kuitazama post hiyo ya Drake hapa.
No comments