Nicki Minaj afunguka maisha yake akiwa”SINGLE” kwa mara ya kwanza
Katika jarida la Elle staa maarufu katika game ya rap nchini Marekani Nicki Minaj amefunguka kuhusiana na kesi iliyomkabili aliyekuwa mpenzi wake Meek Mill na kufunguka pia kuhusu maisha yake ya kuwa single kwa mara ya kwanza tangu akiwa na umri wa miaka 15.
Nicki Minaj na Meek Mill waliachana mwanzoni wa mwezi January 2017 baada ya kuwa wote kwa kipindi cha miaka miwili, Nicki alifunguka na kusema kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa single kwa muda mrefu tokea awe na umri wa miaka 15 baada ya kuachana na Meek na muda huo ulimpa nguvu kufanya maamuzi mengi katika maisha yake ikiwemo pia katika maisha ya muziki.
Nicki alifunguka pia katika jarida hilo na kuongelea kuhusu kifungo cha Meek Mill na kusema kuwa alisikitishwa na phase aliyoipitia Meek na hamuombei yoyote kupitia maisha ya jela kama hayo.
No comments