Drake kutomjibu tena Pusha T
Huenda watu wengi walikuwa wanategemea kusikia majibu ya Drake baada ya rapper Pusha T kutoa diss track ambayo inamzungumzia Drake kumtelekeza mtoto wake ambaye alizaa na stripper sasa habari mbaya ni kwamba kwa mujibu wa Dj Akademiks, Drake hatomjibu tena Pusha T.
Kupitia maongezi ambayo Dj Akademiks anasema kuwa amefanya na Drake, Rapper huyo wa God's Plan ameamua kutulia kwasababu anaamini ya kwamba angeendelea na bifu hilo kungempelekea Drake kwenda sehemu ya kinyama ambayo ingekuwa ngumu kwa kurudi katika mfumo wa amani. Kama utakumbuka hata Jay Prince alishawahi kufunguka kuwa akaushe asiitoe hiyo diss track mpya kwasababu inaweza kuwa balaa.
Ishu kubwa ni kungojea kuona ujazo wa album yake mpya ya Scorpion utakuwaje na unafananaje.
No comments