Breaking News

Cardi awashangaza mashabiki. Aingia kwenye stage na ujauzito na mpenzi wake Offset


Cardi B ameweza kuwa surprise mashabiki wake baada ya kuingia kwenye stage kwa kushtukiza katika show aliyokuwa akifanya mchumba wake Offset akiperform wimbo wa Motorsport huku akiwa ni mjamzito. 

Wawili hao waliungana kufanya show hiyo ya kituo kimoja cha redio nchini marekani maarufu kama Hot 107.9. Mashabiki walioneshwa kufurahishwa sana na msanii huyo wa kike kwasababu ni kitu ambacho hawakujitegemea kwasababu msanii hajafanya show muda mrefu ikiwa ni kwasababu ya hali yake ya ujauzito. Wawili hao watakuwa wanatazamia kupata mtoto wao wa kwanza siku za karibuni.

Cardi B alionyesha kuwa ni mwenye furaha sana baada ya kupewa mic na kuwashangaa jinsi mashabiki wake walivyokuwa wamemmiss msanii huyo. Cardi alikuwa amevalia gauni zuri jeupe lenye maua mekundu ambalo liliweza kumruhusu msanii huyo kufanya show pasipo kumsumbua akiwa na mpenzi wake pembeni yake. 

Unaweza kuwatazama wawili hao wakiperform hapa chini na shangwe za mashabiki wao:

No comments