Liverpool watarajia kumsaini Alisson kwa ada ya £57 milioni
Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa bado anatazamia kumsajili mlinda mlango wa klabu ya AS Roma Alisson ambaye pia ni mlinda mlango namba moja kwenye timu ya taifa ya Brazil. Klopp alisema hayo baada ya matumaini ya kumnyaka mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak kuingia gizani.
Liverpool wanatarajia kuandaa kitita cha £57 milioni ili kuinyaka saini ya mlinda mlango huyo sambamba na kumsajili Shaqiri kutokea klabu ya Stoke City kwa ada ya £13 milioni.
Alisson pia ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa Brazil Ederson, amesema kuwa atasema hatima yake kabla ya kuanza kwa kombe la dunia kuwa ataelekea klabu gani baada ya maisha yake ya Italia.
No comments