Breaking News

Kocha wa Costa Rica amesema kuwa kikosi chake hakitamchezea vibaya staa wa Brazil, Neymar

Neymar alitoka nje kwa ajili ya kupata matibabu ya haraka katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Switzerland lakini kocha wa Costa Rica amesema kuwa hawatamchezea vibaya mchezaji huyo.

Neymar inabidi asihofu kuhusu kuumizwa katika mchezo wa leo ambapo Brazil watacheza dhidi ya Costa Rica hapo baadae alisema kocha wa Costa Rica. Neymar alichezewa faulo mara 11 katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Switzerland, ambayo ni mara nyingi zaidi ya mchezaji yoyote katika mashindano hayo. Mara ya mwisho mchezani kuchezewa faulo mara nyingi hivyo ilikuwa ni mwaka 1998 (Alan Shearer)
"Neymar ni mchezaji mbunifu sana, na nimeona baadhi ya wachezaji wakijaribu kumchezea vibaya ili kuweza kumdhibiti mchezaji huyo. Lakini sisi tuna mipango yetu, na nadhani naweza nikamwekea watu wawili wa kumwangalia lakini hatutaki kumchezea vibaya." Alisema kocha wa Costa Rica.

Brazil watatakiwa kushinda mechi yao ya leo ili kujihakikishia nafasi nzuri katika hatua ya mtoano (16 bora) baada ya kutoa sare katika mechi yao ya kwanza. 

No comments