Breaking News

Ariana Grande na Pete Davidson wachumbiana


Siku chache tu baada ya kufahamu kuwa Ariana Grande anatoka kimapenzi na Pete Davidson baada ya wawili hao kuamua wao wenyewe kuweka wazi mahusiano yao, habari zilizofufikia ni kwamba wawili hao wameshachumbiana. Wawili hao walianza kuongelea hayo hivi karibuni na hivyo hawakuwa na chochote walichokuwa wakikificha.

Chanzo kimoja cha habari pia kilisema kuwa wawili hao waliwatangazia watu waliokuwa wamekuja kwenye sherehe katika nyumba ya msanii mwenzao Robert Pattison, na kuwajulisha kuwa wawili hao wameshachumbiana. 

Pete ambaye ni mchumba wake Ariana hivi majuzi alipngeza tattoo mbili katika mwili wake ambazo zilikuwa zikimhusu mpenzi wake huyo na pia wawili hao wamekuwa wakitoa taarifa mbalimbali kwa mashabiki wao katika mtandao wa Instagram, ikiwemo kujibu maswali ya mashabiki wao ambao huwa wanawauliza kwenye comments.

No comments