Breaking News

Nicki Minaj aungana na Lil Wayne kutoa nyimbo mpya

Baada ya kutangaza ujio wa tour yake na Future, Nicki Minaj amewaambia mashabiki zake pia kuhusiana na collabo yake aliyofanya na Lil Wayne inayokwenda kwa jina la "Rich Sex". 


Nyimbo hii inafanana jina na ngoma ya Future iliyokuwa kwenye album ya "DS2". Nicki amesikika akichana sana kwenye ngoma hii pamoja na mwenzake Lil Wayne. 

Kwa kuongezea tu kwa mashabiki wake kuhusu nyimbo hiyo ya Rich Sex" aliyomshirikisha Lil Wayne, Nicki Minaj pia alitangaza kuhusu nyimbo yake nyingine aliyoimba na Ariana Grande inayokwenda kwa jina la "Bed" ambayo inatoka Juni 14, 2018. Nicki ameendelea kurusha video mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na Ariana Grande mara kwa mara kwa hivyo mashabiki wameendelea kukaa chonjo kuwasikilizia wawili hao kuhusu project yoyote mpya.
Nicki pia ameendelea kupromote album yake "QUEEN" ambayo tayari alishaweka wazi cover ya album hiyo wiki iliyopita. Lakini kwa bahati mbaya album hiyo itachelewa kidogo sio kama ilivyokusudiwa, hivyo itatoka Agosti 10 na sio Julai 15 kama ilivyokuwa hapo mwanzo. 

No comments