Ronaldo aiunga mkono Brazil kushinda Kombe la Dunia
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldo De Lima, ameunga mkono kikosi cha Brazil na kusema kwamba ina nafasi kubwa ya kushinda Kombe la Dunia mwaka huu baada ya miaka 16.
Kikosi hiko kinachoongozwa na Tite, kimeonesha uwezo mkubwa sana katika maandalizi ya Kombe hilo huku katika kundi lao wanatarajia kukutana na Switzerland, Costa Rica na Serbia katika kundi E.
"Kwangu mimi nadhani kwamba Brazil ndo timu pekee ambayo nadhani itafanya vizuri sana, sio kwamba kwasababu mimi pia ni mbrazil lakini nimeona uwezo wao na unanishawishi kwamba wataweza kufanya vizuri sana". Ronaldo ambae alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo mwaka 2002 aliongea na vyombo vya habari jijini Moscow.
"Spain nao pia wanacheza vizuri sana, na Ujerumani siku zote huwa wanacheza kwa nguvu. Lakini Kombe la Dunia ni pambano kubwa sana na ni gumu lakini pia kuwa Argentina ambao wanacheza vizuri pia, na Ufaransa wana kikosi cha vijana wengi sana."
"Natumaini Brazil itashinda. Ni muda mrefu tangu 2002, takribani miaka 16 na nadhani sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo"
Brazil ambao ni mabingwa wa kombe hilo mara tano watafungua mechi yao ya kwanza dhidi ya Switzerland Juni 17, 2018 siku ya Jumapili
No comments