Ujerumani washindwa kutamba mbele ya Mexico, Brazil yashindana nguvu na Switzerland
Mabingwa watetezi Ujerumani hapo jana siku ya Jumapili walishindwa kutamba mbele ya Mexico baada ya kufungwa kwa bao moja na mabingwa hao watetezi kushindwa kurudisha bao hilo. Bao hilo lilifungwa na Hirving Lozano dakika ya 35 ya mchezo akipewa assist na Javier Hernà ndez.
Mexico wamekutana na Ujerumani mara 11 na wamepata ushindi mara moja tu wakiwa wamepata sare mara 5 na wamefungwa mara 5. Lakini jana ufundi wa wajerumani hao wakiongozwa na Manuel Neuer, Thomas Müller, Tony Kroos na Sami Khedira waligonga mwamba kwa waamerika hao wa kusini.
Huku mabingwa wengine Brazil ambao ndio chaguo la mashabiki wengi katika Kombe hili walishindwa pia kutamba mbele ya Switzerland baada ya kupata sare ya bao 1 - 1.
Goli la Brazil lilifungwa na Staa wa klabu ya Barcelona Philipe Coutinho mnamo dakika ya 20 ya mchezo huku bao la Switzerland likifungwa na Steven Zuber dakika ya 50 ya mchezo akiwa amepewa assist na Xherdan Shaqiri. Baadhi ya wasanii walijitokeza kuishangilia timu hiyo akiwemo staa wa miondoko ya Pop Rihanna akiwa na jezi ya Neymar.
Brazil sasa anashika nafasi ya pili katika kundi E akiwa na point 1 na goli moja la kushinda na moja la kufungwa huku vinara wa kundi hilo wakiwa ni Serbia wenye point 3 na bao 1 la kushinda.
No comments