Breaking News

Urusi yafungua vyema mashindano ya Kombe la Dunia kwa kishindo

Timu ya taifa ya Urusi wakiwa ni wenyeji wa mashindano makubwa duniani ya Kombe la Dunia, hapo jana wameweza kuipiga kipigo cha mbwa timu ya taifa ya Saudi Arabia kwa mabao 5 - 0. 
Urusi imejipatia mabao yake matano kutoka kwa wachezaji, Yury Gazinsky aliyetupia dakika ya 12, Denis Cheryshev akitupia dakika ya 43, 90+1, huku Artem Dzyuba akifunga dakika ya 71 na Aleksandr Golovin akihitimisha karamu hiyo ya mabao dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika.
Mpaka sasa hakuna timu yoyote mwenyeji iliyowahi kupoteza mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe na timu ya taifa ya Urusi imeendeleza utamaduni huo baada ya kuibuka na ushindi huo mnono dhidi ya Saudia mchezo wa kundi A.

No comments