Wanawake Saudi Arabia waruhusiwa kuendesha magari
Wanawake nchini Saudi Arabia wamenza kuendesha magari nchini mwao kwa mara ya kwanza, baada ya kuondolewa rasmi kwa sheria iliowazuiya kufanya hivyo.
Saudi Arabia ilikuwa nchi ya mwisho duniani, ambapo wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuendesha magari. Ni hatua ya kihistoria kwa wanawake wa nchi hiyo, ambao walikuwa wakilazimika kutegemea jamaa zao wa kiume au kuajiri madereva katika usafiri wao wa kila siku katika shughuli za maisha.
Wanawake na wanaume wanaowaunga mkono wamekuwa wakiendesha kampeni ya miongo mitatu kupinga sheria hiyo, na wanaharakati wengi wa kike walikamatwa na kufungwa jela walipojaribu kuikiuka sheria hiyo.
No comments