Marekani yawaunganisha na familia zao, watoto wahamiaji 522
Wizara ya usalama wa ndani ya Marekani imesema imewaunganisha tena watoto 522 na familia zao, walizokuwa wametenganishwa nazo katika mpango wenye utata wa kuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Mpango huo wa utawala wa Rais Donald Trump ulilaaniwa vikali ndani na nje ya Marekani. Taarifa za hivi karibuni zimeeleza kuwa Wizara ya Afya na huduma za binadamu ilikuwa imewatenganisha watoto 2,053 kutoka familia zao na kuwapeleka katika vituo vinavyoendeshwa na wizara hiyo.
Malalamiko yaliyotangazwa kupitia vyombo vya habari, yalisema baadhi ya wazazi hawakuwa na mawasiliano yoyote na watoto wao walio katika vituo hivyo.
Katika tangazo lililotolewa jana jioni, wizara ya usalama wa ndani ilisema idadi ndogo ya watoto ambao kutenganishwa kwao na familia zao hakukutokana na sera ya kutoruhusu yeyote kujipenyeza nchini Marekani, hususan wale ambao uhusiano wao na familia hizo haueleweki vyema, wataendelea kuhifadhiwa katika vituo vivyo
No comments